Monday, 3 March 2014

JACKSON KISWAGA AMPONGEZA RAIS KIKWETE KULINDA AMANI NCHINI, AKABIDHI MSAADA WA SARUJI KKKT KIDAMALI

Hili  ndilo kanisa ambalo Kiswaga  ametoa msaada wa  Saruji


Waumini wa kanisa hilo  wakishusha  Saruji katika gari la Kiswaga
Kiswaga  akizungumza na  waumini hao  baada ya  kuwakabidhi msaada wa  Saruji
Mkazi  wa kijiji  cha Nyamihuu jimbo la Kalenga Bw Jackson Kiswaga
kulia akikabidhi msaada wa mifuko 10  ya  saruji  Bw Aidan Nyato
mwenyekiti wa  baraza la  wazee wa  Kanisa la kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) usharika wa Kidamali  jimbo la Kalenga
Mkazi  wa kijiji  cha Nyamihuu jimbo la Kalenga Bw Jackson Kiswaga
kulia akikabidhi msaada wa mifuko 10  ya  saruji  Bw Aidan Nyato
mwenyekiti wa  baraza la  wazee wa  Kanisa la kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) usharika wa Kidamali  jimbo la Kalenga
Kiswaga  akizungumza na  waumini hao  baada ya  kuwakabidhi msaada wa  Saruji
…………………………………….
Na Francis Godwin Blog 
MKAZI wa kijiji  cha Nyamihuu aliyekuwa  mshindi wa  pili katika  kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa  kugombea  ubunge jimbo la Kalenga  kupitia chama  cha mapinduzi (CCM) Bw Jackson Kiswaga ametoa msaada  wa  saruji mifuko 10 kwa  uongozi wa kanisa la kiinjili  la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika  wa Kidamali wilaya ya Iringa mkoani hapa huku  akiwataka watanzania wenye uwezo kuendelea kuchangia nyumba za ibada kama njia ya kulinda amani yetu.  

Huku akimpongeza Rais Dr Jakaya  Kikwete  kwa  kuendelea kuongoza nchini  kwa hali ya amani na utulivu kwa  kila mtanzania kufanya shughuli  zake bila kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani kama zilizo nchi nyingine barani Afrika.
Akizungumza   wakati wa  kukabidhi msaada  huo  leo Kiswaga  alisema  kuwa ametoa msaada  huo  kufuatia maombi ya  uongozi wa kanisa  hilo  kwake  na  kuwa kama mmoja kati ya  waumini wa Kanisa hilo aliguswa na  jitihada za
waumini  hao kutaka  kumjengea  nyumba mchungaji  wao.
 
Hivyo msaada  huo  utasaidia kuanza  ujenzi  wa nyumba hiyo ya mchungaji na  kuwa ataendelea  kuchangia hatu  moja  hadi nyingine katika  ujenzi huo huku  akiwataka  waumini  wengine wa kanisa  hilo a  wale ambao si waumini wa kanisa  hilo  kuendelea  kujenga utamaduni wa  kuchangia nyumba za ibada    ili  ziweze kutumika katika kuliombea Taifa amani zaidi .
 
Alisema iwapo watanzania  wataelekeza nguvu zao katika ujenzi wa  nyumba za ibada nchi  itaendelea  kuwa na wananchi  wacha Mungu na  wasiopenda  kuona  amani  inachezewa .
 
Kiswaga  alisema  kusaidia nyumba  za ibada  mbali ya kumwezesha  mchangaji  kupokea  baraka  za Mungu katika shughuli  zake ila bado ujenzi  huo wa  nyumba za ibada utachangia watu  wachache  ambao  hawana mazoea ya kwenda katika nyumba za ibada kama Makanisani na Misikitini  kushawishika na kumgeukia Mungu.
 
“Nyumba  za  ibada ni  sehemu ya  baraka  hivyo lazima watanzania  kuendelea kuchuma  baraka  kwa  kuchangia nyumba za ibada”
 
Akishukuru  kwa msaada  huo  mwenyekiti wa  baraza la  wazee kanisani  hapo Aidan Nyato alisema  walilazimika  kumwandikia  barua Kiswaga na kumuomba msaada  wake  kutokana na jitihada  mbali mbali ambazo amekuwa akionyesha katika kuwaletea maendeleo  wananchi wa kijiji  hicho na maeneo mengine .
 
Alisema hadi sasa  bado kanisa  hilo linaomba kusaidia msaada wa mbao  zaidi ya 100 bati 150 ili  kukamilisha ujenzi wa nyumba  hiyo ya mchungaji .

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!