Baada ya mivutano na malumbano ya makundi ya wajumbe hatimae bunge maalum la katiba limepitisha rasimu ya kanuni za kuongoza bunge hilo huku vifungu vya 37 na 38 vikiachwa kiporo kutokana na kutofikiwa kwa makubalino.
Akizungumza baada ya kupitishwa kwa rasimu hiyo mwenyekiti wa muda bunge Mhe. Pandu Ameir Kificho amewataka wajumbe wanaotoka kuchukua fomu za kugombea nafasi ya wenyekiti kuchukua fomu hizo na kusistiza uchaguzi wa mwenyekiti wa kudumu wa bunge la katiba utafanyika Machi 12 mwaka huu saa kumi jioni na makamu mwenyekiti utafanyika baada ya kupatikana mwenyekiti wa kudumu kwa kuzingatia sheria Mhe. Pandu Ameir Kificho - mwenyekiti wa muda wa bunge la katiba.
Awali wakizungumza katika semina hiyo viongozi vya vyama vya siasa wamesisitiza umuhimu wa wajumbe kuwa umoja unatawezesha kujenga makubaliano wakati wa majadiliano yatakayoweza kufikiwa mwafaka utakaosaidia kupata katiba mpya.
Baadhi ya viongozi wa dini waliopata fursa ya kuzungumza katika semina hiyo, wamesema mivutano na migogoro iliyojitokeza wakati kupitisha rasimu ni mapungufu ya kibinadamu.
Wakizungumza na itv nje ya ukumbi wa bunge baadhi ya wajumbe wamepongeza hatua ya kupitishwa kwa rasimu na kuainisha changamoto zitakazojitokeza katika mijadala ya katiba kutokana na kuwekwa viporo kwa vifungu vya 37 na 38 vinavyofafanua namna ya kufanya maamuzi
No comments:
Post a Comment