Tuesday, 11 March 2014

FAHAMU MTI WA MAAJABU (MLONGE) UNATIBU ZAIDI YA MAGONJWA 300





KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge unaweza kuwa unaongoza. Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.


Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja lijulikanalo kama Trees For Life, majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.
Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma  (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.

Ili kutengeneza ‘tonic’, saga majani mabichi ya Mlonge pamoja na maji, yachuje kisha changanya na maziwa halisi. Inaelezwa kuwa juisi ya aina hii ni dawa nzuri kwa waja wazito, kwani huboresha njia ya uzazi na kumuwezesha mama kuzaa bila matatizo na kuondoa matatizo baada ya kujifungua.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu, baadhi yake ni kama haya yafuatayo:
Mlonge unaweza kutibu Pumu, Kikohozi na Kifua Kikuu. Aidha, magonjwa mengine kama Kisukari, Shinikizo la damu (la juu na chini), magonjwa ya ngozi, magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI) kuongeza kinga ya mwili (CD4) na kuongeza nguvu za kiume




Unga wa majani ya Mlonge ambao ni lishe, tiba na kinga hutibu magonjwa kama shinikizo la damu,kupooza viungo au kufa ganzi,homa ya matumbo(typhoid),kuwashwa mwili,vidonda vya tumbo,malaria sugu, enia, upele n.k.Mbegu za Mlonge hutibu Malaria, Saratani ya tumbo,hupungusa sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji,huongeza kinga ya mwili CD4s. (Tumia mbegu 3x3 muhimu kila ukitafuna mbegu tatu kumbuka kutumia maji glass 3 au zaidi)
Maganda(magome) ya Mlonge husaidia kusafisha maji(water treatment).
Mizizi hutumika kutibu watu walio na malaria sugu au watu wanaopata homa ya usiku au wanaotiririka sana jasho wakati wa homa. Mizizi hutumika kwa kusaga unga wake na kutumia kijiko cha chai mara tatu kwa siku.
Dozi ya Ukimwi. Dozi ya ukimwi ni kutumia unga wa majani kijiko cha chai mara tatu kutwa kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita. Pia mgonjwa anatakiwa kutafuna mbegu tatu mara tatu kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita.
Unahamasishwa na kushauriwa angalao nyumbani kwako uwe na mashina kadhaa ya mmea huu kwa matumizi yako

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!