ASKARI wa magereza wa jela la Taveta Boniface Muriithi amemuua kwa kumpiga risasi mwenzake kwa jina Livingstone Sowene.
Tukio hilo limetokea leo saa mbili asubuhi ya Jumanne lilitokea nje ya gereza hilo wakati Muriithi alipoamua kummiminia mwenzake risasi tano kwenye kifua bila kumuuliza chochote.
Wawili hao hata hivyo wamekuwa na uhasama ambao unadaiwa kuzidi baada yao kupangwa wafanye kazi katika shifti moja.
Mkuu wa gereza hilo Bw Soud Ramadhan amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamemnasa mwenzao huyo na kumkabidhi kwa polisi ili afunguliwe mashtaka.
“Muriithi alimkuta Sowene akisubiri kupeleka wafungwa kazini alipompiga risasi tano kifuani, alikufa akiwa ameketi papo hapo. Ni jambo la kushangaza kwa hata hawakuongea ndiposa tujue kama palikuwepo uhasama wowote,” akasema askari huyo.
Duru hata hivyo zinasema mshukiwa alijawa na ghadhabu baada ya kupashwa habari kwamba askari huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe.
Jamii na rafiki wa marehemu wamelalamika kumpoteza mmoja wao kwa njia katili ya kuangamizwa na mfanyakazi mwenzake.
Babake marehemu Bw Joseph Sowene amesema kuwa mwanaye aliamkia kumpeleka bintiye shuleni na mkewe shuleni Makloriti anakofunza.
“Tumetatizika pakubwa kwa kuwa aliyeuawa ni mzazi mchanga aliyejali sana jamii yake. Hatujui kilichosababisha hili na tunataka polisi watuambie kilichotokea,” akalalama mzazi.
Mkuu wa polisi wa Taita Taveta Richard Bitonga alithibitisha kisa hicho na kusema uchunguzi unaendelea kubaini kiini hasa cha mauaji hayo.
Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Taveta akisubiri kufikishwa mahakamani karibuni.
Crd: paparaz.
No comments:
Post a Comment