Tumeshuhudia miezi miwili ya vuta ni kuvute kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wafanyabiashara nchini ambao walifunga biashara zao ili kuishinikiza Serikali kutatua changamoto kwenye mashine za Electronic Fiscal Device (EFD) na taratibu za kutoa mizigo bandarini pamoja na vikwazo vingine.
Wafanyabiashara hao walilazimika kufunga shughuli zao za biashara kutokana na vikwazo vitano ambavyo ni; mazingira mabovu ya kufanya biashara, kiasi cha kodi wanachotozwa, rushwa, kero za mashine za EFD ambazo zinatumika kutoa risiti na kuweka kumbukumbu za kodi na utawala mbovu katika kusimamia suala zima la kodi.
Kutokana na kuwapo kwa hali hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Jonson Minja anasema vikwazo hivyo vinapaswa kufanyiwa kazi na mamla husika wakiwamo watendaji wa kuu wa TRA na serikali kuu.
“Unajua, jamii imepotoshwa kwamba wafanyabiashara wanakataa kutumia mashine za EFD kwa sababu ni kawaida yetu na tumezoea kukwepa kulipa kodi, lakini ukweli ni kwamba kuna mambo mengi ambayo Serikali inapaswa kuyatatua kuhusu mashine hizi. Lengo ni Serikali inufaike pamoja na sisi wafanyabiashara,” anasema Minja.
Wafanyabiashara hao wanasema, lengo lao ni kujenga mazingira ambayo wengi watashawishika kulipa kodi kwa urahisi na anayepaswa kufanikisha hilo ni Serikali.
Moja ya mambo yanayowakwaza wafanyabiashara hao ni rushwa na usimamizi mbovu wa kukusanya kodi. Mambo hayo ndiyo yanayosababisha wagome kutumia mashine hizo kwa sababu hakuna uwiano wa kodi wanayotozwa na wanayolipa kupitia mashine hizo. Pia kikwazo kingine ni kukatika kwa umeme jambo ambalo wanalazimika kutoa taarifa TRA kwanini mashine za EFD haikutumika au kwanini ilizimwa.
Minja anasema kutokana na rushwa kuchukua nafasi kubwa katika Bandari ya Dar es Salaam, wafanyabiashara wamekuwa wakilazimika kutaja thamani ndogo ya mizigo wanayoiagiza kutoka nje ili kukabiliana na mfumo mbovu wa kutoza kodi bandarini.
“Hakuna vigezo vya kisayansi kwa ajili ya kutoza kodi bandarini, kazi ya kutoza kodi inafanywa na maofisa wa TRA kwa kuangalia kwa macho na kukadiria mteja anapaswa kutozwa kiasi gani cha kodi, anasema Minja.
Minja anasema njia ya kukadiria mizigo bandarini, ni hatari kwa uchumi wa taifa letu kwa kuwa hakuna vigezo maalumu vya kutathimini bidhaa mbalimbali zinazoingizwa nchini.
Jambo lingine, Minja anasema ni vigumu kutumia mashine za EFD kwa kuwa wafanyabiashara wengi wanatumia kontena moja kuagiza mizigo kutoka nje ambalo linawajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 50 kutokana na kutokuwapo kwa mfumo rafiki wa kutoa mizigo bandarini.
Anasema wakati wa kutoa mizigo bandarini, jina moja kati ya wafanyabiashara hao ndilo linaloandikishwa kwenye nyaraka za kutolea mizigo. “Hii inamaanisha kwamba wafanyabiashara wengine 49, hawatakuwa na nyaraka za kuagizia mizigo, hivyo itakuwa vigumu kutumia mashine ya EFD,” anasema Minja.
Lakini Kayombo anasema ni hatari kwa wafanyabiashara wengi kutumia kontena moja na jina la mtu mmoja wakati wa kuagiza bidhaa nje ya nchi
MWANANCHI..
No comments:
Post a Comment