Hapa ilikuwa ni pata shika ambapo dada huyo amewekwa kati huku vijana wa eneo hilo wakiwa wanapiga kelele huku wakimvua nguo na kumfanyia vitendo visivyo vya kibinadamu
Anaeonekana kwa mbali ni mdada ambaye alijitolea kwenda kumsaidia dada huyo ambae alikuwa amevaa kanguo kafupi ka nusu utupu akikatiza maeneo kituo cha basi cha mwenge usiku huuHapa akiwa amevuliwa nguo na baadhi ya kina mama kumsaidia na kumwingiza katika gari moja wapo ili kumsitili
Umati wa watu ukiwa umeongezeka na kuzingira basi hilo la abiria na kudai ashushwe ili waweze kumchapa na viboko kwa kitendo cha kuwadhalilisha akina dada wengine
Angalizo: Hatukuweza kuweka picha za binti huyo akiwa mtupu kulingana na maadili.
KWA MTAZAMO WANGU, HILI NI TATIZO SERIKALI LAZIMA IINGILIE KATI, HUU NI UONEVU NA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAWAKE, SIONI SABABU YA WANAWAKE KUZOMEWA, NA KUTENDEWA KAMA HUYU ALIVYOTENDWA, HIYO NI TAMAA YA WANAUME NA SI KOSA LA MWANAMKE..KILA MTU ANA UHURU NA MAISHA YAKE, WE KAMA UNATAMAA ZAKO, HILO NI TATIZO LAKO, AMBALO UNATAKIWA UTAFUTE UFUMBUZI, MBONA MNATUNYANYASA HIVYO? KHA!
Picha na Dar es salaam yetu
No comments:
Post a Comment