Tuesday 25 February 2014

DAKTARI FEKI ANASWA MUHIMBILI

Kuhusu Daktari feki aliyekamatwa Muhimbili leo.

Leo February 25 Uongozi wa hospitali ya
taifa muhimbili kwa kushirikiana na maafisa wake wa usalama wamemnasa
 daktari feki aliyekuwa akiwatapeli fedha wagonjwa na watu mbalimbali 
wanaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo.



Taarifa kutoka Muhimbili inasema ni Tukio la tatu kutokea katika hospitali
 hiyo ingawa matukio ya namna hiyo yameshawahi kuripotiwa katika
 baadhi ya hospitali kubwa za serikali kwa baadhi ya watu wanaotumia
 mwavuli wa fani ya udaktari kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Msemaji wa Hospital ya taifa Muhimbili Aminieli Aligaesha amemtaja Daktari huyo feki kwa jina la Kitano Mustapha na kubainisha kuwa katika upekuzi uliofanywa na maofisa usalama wa hospitali hiyo wamemkuta mtuhumiwa akiwa na kadi tatu za kliniki,namba za simu za madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria zilizopo na kanuni za utabibu.

Daktari huyo feki Kitano Mustapha amekana kutohusika na utaperi huo
 kwa wagonjwa mbali mbali wanaofika kupata huduma za kimatibabu 
na kusema hawezi kuongea lolote mpaka Mwanasheria wake awepo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!