Friday, 3 January 2014

WACHINA TENA! WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO 81 BANDARINI DAR ES SALAAM- JAN 02, 2014




Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na vyombo vingine vya Dola, tarehe 2 Januari 2014 majira ya saa tatu asubuhi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, imekamata meno 81 ya tembo yenye uzito wa kilo 303 sawa na tembo 41. Aidha, magamba 120 ya kakakuona na mazao ya bahari nayo yamekamtwa.

 Hii ni baada ya Askari wa Bandari kutilia shaka mizigo iliyokuwa kwenye gari ikiingizwa bandarini. Meno ya tembo yaliyokamatwa bado ni mapya ikiwa na maana tembo hao wameuawa katika kipindi kizichozidi mwezi mmoja uliopita.
Wizara inasikitishwa sana na vitendo hivi viovu vya ujangili ambavyo vimetokea ndani ya muda mfupi. Tayari watuhumiwa wawili wanashikiliwa na Polisi kufuatia tukio hilo. Majina yao yanahifadhiwa kwa lengo la kutovuruga upelelezi.
Serikali inasisitiza tena kwamba imejizatiti kupambana na vitendo vya ujangili katika mapori yote na maeneo yote ya mipaka ya nchi yetu. Pia, Serikali inapanua wigo wa upelelezi kuhakikisha wote waliohusika wanapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Imetolewa na:


Chikambi K. Rumisha

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!