Sunday, 5 January 2014

STEVE NYERERE AWA MWENYEKITI WA BONGO MOVIE


Pichani
ni Uongozi wa juu wa  Chama cha Wasanii wa Filamu hapa nchini.a.k.a
Bongo Muvi,kulia ni Katibu Mkuu,William Mtitu,Mwenyekiti,Steven
Mengere a.k.a Steve Nyerere,Katibu Msaidizi Bi.Devotha Mbaga,Mweka
hazina Mkuu, Issa Mussa Cloud pamoja na Makamu Mwenyekiti ,Mahsein Awadh
maarufu kama Dk Cheni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kuchaguliwa hapo jana na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo waliokutana
kwenye viwanja vya Lidaz club,jijini Dar.

Pichani
ni Mwenyekiti wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi,
Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika
wadhifa huo wa uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka
kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia
yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa
filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii
wake wananufaika na  kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa
ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na
Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa.
Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania
haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika
kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu.
Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond
peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu,Dk Cheni akiwashukuru wadau
mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine
kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa
ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama
hicho
Katibu Mkuu wa
Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi,William Mtitu akizungumza
machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika suala zima
la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao watahakikisha chama chao kinasimama imara.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo
Muvi,Vincent Kigosi a.k.a Ray akitoa shukurani kwa wanachama na wadau wa
tasnia yao waliofika kwenye uchaguzi huo,Ray amewataka viongozi hao
wapya kuendelea kuijenga tasnia hiyo katika suala zima la kuhakikisha
inaendelea kukua siku hadi siku.
Ray akifafanua jambo kwa ufasaha mara baada ya kukabidhi nafasi yake ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya Steve Nyerere.
Picha ya pamoja
Mwenyeki wa Bongo Muvi Steve Nyerere na Mdau wa filamu hapa nchini wakiwa katika picha ya pozi.
Baadhi ya Wasanii wa Bongo Muvi wakifuatilia mchakato wa uchaguzi wa viongozi wao.
Waratibu
wa Uchaguzi huo wa viongozi wa chama cha wasanii wa filamu nchini
wakiongozwa na Mama Asha Baraka wakihesabu kura za washiriki
waliongombea nafasi mbalimbali katika chama hicho.
Mratibu
wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa chama cha Wasanii wa Filamu,Mama
Asha Baraka akitoa muongozo na kuzungumza machcahe kuhusiana na uchaguzi
huo.
Sehemu ya Wagombea wakisikiliza matokeo yao,William Mtitu,Steve Nyerere,Dada Wastara pamoja na Dk Cheni.
Baadhi ya Wasanii wa Bongo Muvi wakifuatilia mchakato wa uchaguzi wa viongozi wao.PICHA ZOTE NA MICHUZI MEDIA GROUP.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!