Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. JAKAYA KIKWETE amewaapisha Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi JAFARI OMARI na Balozi atakayeiwakilisha Tanzania nchini Malaysia Dkt. AZIZI MLIMA.
Kiapo hicho kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kimeshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu BENJAMIN WILLIAM MKAPA na mke wake Mama ANNA MKAPA.Baada ya kuapishwa viongozi hao wameahidi kutekeleza kikamilifu majukumu watakayopangiwa kuyafanya kwa maslahi ya nchi.Katika hatua nyingine Rais wa Kikwete amemsifu na kumpongeza Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, BENJAMIN MKAPA kwa kuchangia historia ya Tanzania kupitia uamuzi wake wa kuchapisha vitabu vya hotuba zake alizozitoa wakati wa uongozi wake wa miaka 10.
Pongezi hizo amezitoa baada ya kupokea nakala za vitabu vya hotuba za miaka 10 ya uongozi wa Rais Mkapa, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.
Pongezi hizo amezitoa baada ya kupokea nakala za vitabu vya hotuba za miaka 10 ya uongozi wa Rais Mkapa, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment