Wednesday, 8 January 2014

KUFUATIA MWANAMKE KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA, DR. MWAKYEMBE ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM


Mhe. Mwakyembe.
KITENGO  Cha Usalama wa Taifa Nchini kinatarajia kuogeza nguvu katika kuimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege nchini ili kukabiliana na wimbi kubwa la usafifirishaji wa dawa za kulevya pamoja na madini hapa nchini hususani katika kiwanja cha ndege cha kimataifa  Mwalimu Julius Nyerere (JNA) kilichopo jijini Dar es Salaam.

Akiongea  na  menejimenti  ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege katika ofisi za uwanja wa kimatifa
Mwalimu  Julius Nyerere,Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe alisema mipango mikakati ni  pamoja na kushirikisha vyombo vingine, kama vile uhamiaji,polisi , kitengo cha dawa za kulevya nchini, polisi jammii na raia wema wa kawaida watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa matukio ya kupitisha maidini na dawa za kulevya
DK. Mwakyembe alikwenda katika viwanja hivyo kufuatia kuwepo na taarifa ya kukamatwa kwa mwanamke mmoja akiwa na hati ya kusafiria AB548424 aliefahamika kwa jina la  Salama Omary Mzala (30) mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salam, aliekamatwa akiwa amemeza pipi 67 za dawa aina ya heroine.
Vyombo vya usalama  Kumtilia shaka na kuweza kufuatilia hadi katika ndege aliotakiwa kupanda ya Ethpoia Airline  tayari kwa kuelekea Maccau Nchni  China na kumuweka katika ulinzi ambapo kwa mujibu wa taaarifa toka kwa kamanda wa kikosi chamkuzuia na kupamabana na dawa za kulevya nchini Godfrey Nzowa hadi kufikia saa 7.30 mchana ,Mzala alikuwa ametoa pipi 28 kwa njia ya haja kubwa ambapo naendelea kutoa kadri muda unavyozidi kwenda .
Akitoa takwimu za kupitisha dawa na madini kupitia kiwanja hicho Dk. Mwakyembe alisema  vitendo vya kutorosha madini kuanzia Oktoba hadi December kesi 14 zililipotiwa wakati kuanzia August hadi Desemba mwaka jana matukio nane ya dawa za kulevya yaliripotiwa ambapo watano wa wahusika katika matukio hao ni watanzania.
Akiongea kwa njia ya simu kamanda Nzowa alisema kukamatwa kwa binti huyo kunatokana na kupeana taarifa kiulimwengu ambapo kuligana na teknolojia iliopo hivi sasa mtu anaweza kukamatwa mahali alipo hata kabla ya kusafiri kwende nchi nyigine. Aidha anaunga mkono jitihda za Rais Jakaya Kikwete za kuleta maadiliko makubwa  katika vita vya kuthbiti na kupambana na dawa za kulevya nchini ili kukomesha biashara hiyo.
Alitoa angalizo kwa wananchi kutojiusisha na kilimo cha aina yoyote ya dawa za kulevya badala yake wageukie kilimo cha mazao ya biashara na chakula. 
Alitoa takwimu ya dawa za kulevya zilizokamatwa  nchini Kamanda Nzowa alisema Mwezi wa saba pekee kilo 182 za heroine zilikamatwa na hadi kufikia mwisho wa mwaka jana  jumla ya kilo 1482 za heoroine zilikamtatwa kitu ambaho na hatari. “tunaendelea kupambana hadi kukomesha kwa biashara hizi kwani watu hawa (wafanyabiashara ni wajanja sana hubadilisha mbinu kila wakati na sisi hatulali”alisema Kamanda Nzowa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!