Sukari |
Wengi wetu tumeshasikia ushauri wa kula sukari kidogo, ushauri ambao ni mzuri kiafya.
Lakini licha ya tahadhari mbalimbali zinazo tolewa na wataalamu wa afya kuhusu madhara yatokanayo na ulaji mwingi wa sukari, bado idadi kubwa ya watu hupenda kutumia sukari kwa wingi kwa njia mbalimbali.
Utumiaji wa sukari siyo lazima ile sukari nyeupe
( white ) au kahawia ( brown ) pekee, bali pia hata sukari asilia inayo patikana kwenye matunda, maziwa, asali, vinywaji baridi, pombe, baadhi ya nafaka nakadhalika.
Hizo zote ni aina ya sukari ambazo zinatofautiana faida na madhara.
Wakati viwanda vya uzalishaji sukari duniani vinaongezela, tatizo la unene kupita kiasi kwa biandamu nalo linaendelea kuongezeka.
Sukari inahusika kwa kiasi kikubwa na tatizo la kuongezeka kwa unene wa kupindukia ( obesity).
Kwa watu wanene, ulaji wa sukari hata kijiko kimoja tu kwa siku, huchangia kwenye tatizo.
Sukari ni ya kuepukwa, siyo tu kwa watu wanene, bali hata kwa watu wengine wenye kujali afya zao.
Katika kitabu chake kiitwacho “ LICK THE SUGAR HABIT ‘, Mwanalishe Nancy Appleton ( PhD), ameelezea sababu 146 za kwa nini sukari hudhoofisha afya zetu.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo ;
i. Sukari huweza kuathiri ukuaji wa homoni mwilini ( kitu ambacho ni muhimu kwa kumfanya mtu kuishi na afya njema wakati wote )
ii. Sukari ndiyo chakula cha saratani mwilini.
iii. Sukari huongeza lehemu ( cholesterol ) mwilini.
iv. Sukari huweza kusababisha kizunguzungu na kudhoofisha mwili kwa watoto.
v. Sukari huweza kudhoofisha nguvu ya macho
vi. Sukari huweza kuzuia utembeaji wa protini mwilini
vii. Sukari huweza kusababisha mzio wa chakula ( Food allergies )
viii. Sukari huchangia ugonjw a wa kisukari
ix. Sukari huweza kusababisha ugonjwa wa moyo.
x. Sukari huweza kuharibu, umbo la vinasaba vya mwili ( D.N.A )
xi. Sukari huweza kusababisha utukutu, utundu na kukosa umakini kwa watoto.
xii. Sukari huweza kuchangia kupunguza n kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yatokanayo na wadudu aina ya bacteria ( infectious diseases )
Hizo ni baadhi tu ya hizo sababu 146. Je, kwa kujua sababu zote zilizo thibitishwa kuhusu madhara yatokanayo na sukari, kuna sababu gani ya kuendelea kupenda kutumia sukari ?
Kiasilia, mwanadamu ana ladha sita tofauti zikiwemo za uchungu, utamu, ukali,uchachu, na ukakasi.
Hivyo kuacha kabisa ulaji wa ladha tamu, kunaweza kusababisha madhara mengine ya kibaiolojia na ndiyo maana watu wengi hushindwa kujizuia kutumia sukari, hasa kwa watoto ambao kwao huonekana ni jambo lisilo wezekana kabisa kuacha kulamba sukari.
Hata hivyo, kuna habari njema kuwa unaweza kutumia mbadala wa sukari nna kupata ladha ya utamu katika vinywaji au vyakula vyako bila kuwa na madhara.
Moja ya mbadala wa sukari anaye aminika na wengi tangu enzi na enzi , ni asali, ambayo unaweza kuitumia kwenye vinywaji mbalimbali bila kuwa na madhara.
Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wanasema kuwa asali nayo ina ‘ fructose’ , huenda ikawa na madhara pia, ingawa kwenye vitabu vya dini na baadhi ya wanasayansi wameilezea asali kama kitu kisicho na madhara mwilini licha ya kuwa nayo ni tamu kama sukari.
Sukari ya Stevia |
Baadhi ya wanasayansi wamependekeza zaidi mbadala wa sukari kuwa ni “ Stevia” na “ Xylitol”, ambavyo vinatokana na mimea na majani, lakini vina ladha ya utamu kuliko hata sukari.
Sukari Ya Xylitol |
‘ Stevia’ na ‘Xylitol ‘ hutumika zaidi katika nchi za Ulaya , Japan na Amerika ya Kusini, kwetu Afrika hazijulikani sana na sidhani kama zipo.
Jambo la msingi ni kujua kwamba sukari tunaipenda, lakini sio chakula kizuri kama tunavyo weza kudhani, hivyo tujitaidi kuiepuka kadri tunavyo weza kwa kutumia vyakula mbadala kama asali, pale tunaposhindwa kabisa kuiepuka, basi tutumie kwa uchache sana
No comments:
Post a Comment