Saturday, 4 January 2014
CRISTIANO RONALDO APEWA TUZO YA HESHIMA NCHINI URENO
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ambaye pia anachezea timu ya Real Madrid ya Hispania ametunukiwa tuzo ya heshima ya juu kabisa ya heshima nchini Ureno.
Cristiano (28) atakabidhiwa tuzo hiyo inayojulikana kama “Order of Prince Henry” na Rais wa nchi hiyo Anibal Cavaco Silva katika sherehe itakayofanyika siku ya jumanne ijayo.
"Huyu ni kijana ambaye amekuwa alama ya Ureno, ameifanya nchi yetu ifahamike kimataifa na amekuwa ni mfano hai wa ustahimilivu katika kutafuta mafanikio kwa vijana wa nchi hii,” ilisomeka taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais.
Kwa upande wa Ronaldo, yeye alisema "hii ni heshima kubwa mno kwake kuliko hata anavyostahili. Nimekuwa nafanya kila kitu nikiwa naiangalia nchi yangu nikitegemea kuwa vijana wanaochipukia wanaweza kujifunza lolote kutoka kwangu. Naipenda sana nchi yangu".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment