Thursday, 5 December 2013

WAFANYAKAZI UWANJA WA KIA MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA...


Uwanja wa Ndege wa KIA.
Wafanyakazi wawili wa Kampuni ya Uwakala wa Uendeshaji wa Uwanja
 wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO), wanashikiliwa Polisi
 kwa madai ya kupanga njama za kupitisha wasafirishaji wa dawa za
 kulevya katika uwanja huo.
Jana Polisi mkoani Kilimanjaro ilikamata wafanyakazi hao
  (majina tunayo), kwa tuhuma za kusafirisha hadi uwanjani hapo 
wanawake wawili raia wa nje, wanaodaiwa kukamatwa na dawa 
za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo 15 mwishoni mwa wiki.
Taarifa kutoka katika uwanja huo, zilidai kuwa wafanyakazi hao, ndio 
waliohusika kusafirisha watuhumiwa hao raia wa Nigeria na Liberia mpaka
 katika uwanja huo na walifika saa 9 mchana Jumamosi iliyopita.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka uwanjani hapo, wanawake
 hao wawili walitumia gari aina ya Noah, linalodaiwa kumilikiwa na mmoja
 wa wafanyakazi hao.
Mtoa habari wetu alidai kuwa baada ya kufikisha wageni hao 
uwanjani, mwanamke Mnigeria aliyekuwa na kilo 10 za dawa
 hizo, aliandaliwa mazingira ya kupita uwanjani hapo bila kukaguliwa
 lakini kwa bahati mbaya alikuwa ameshachelewa ndege.
Kutokana na hali hiyo, aliandaliwa usafiri mwingine wa Shirika la Ndege
 la Precision kwenda Nairobi kuanzia saa 11 alfajiri ya juzi.
Mwenzake Mliberia anayedaiwa kuwa na kilo tano za dawa hizo
 aliandaliwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia na alitarajiwa 
kuondoka uwanjani hapo saa tisa usiku wa kuamkia juzi pia.
Taarifa hizo zilidai kuwa wafanyakazi hao kwa kuwa hawakuwa
 zamu usiku, walikabidhi wageni hao kwa mfanyakazi mwenzao 
na kumlipa ili asaidie wapite uwanjani hapo bila kukamatwa.
Hata hivyo, inadaiwa mfanyakazi huyo muda ulipofika, aliondoka eneo
 la kazi na kuaga kwenda kunywa chai na kumwacha mwingine, hatua 
iliyosababisha wakamatwe.
Juzi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
 alithibitisha kukamatwa kwa raia hao wa kigeni na akaahidi angewataja
 majina jana, lakini hakufanya hivyo.
Mwandishi alipomtafuta jana, kupata majina ya watuhumiwa hao na
 kuthibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wengine, simu yake ilipokewa
 na msaidizi wake, ambaye alisema Kamanda Boaz alikuwa katika kikao 
cha ndani asingeweza kuzungumza

GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!