Pilau Ya Tuna Na Mboga
Vipimo
Mchele 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu 1 Mug
(Frozen veg)
Tuna 2 kopo
Thom na tangawizi 2 vijiko vya supu
Garam masala 1 kijiko cha supu
Nyanya 2
Kitungu maji 1
Mdalasini nzima 2 vijiti
Karafuu 6 chembe
Pilipili mbichi 1
Chumvi kiasi
Viazi 3
Maji 2 ½ Mugs
Mafuta 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
- Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
- Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
- Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
- Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
- Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
No comments:
Post a Comment