Friday, 6 December 2013

TANZANIA IMETAJWA KUWA NA VIWANGO VIKUBWA VYA KODI KWENYE MISHAHARA YA WAFANYAKAZI



Tanzania imetajwa kuwa na viwango vikubwa vya kodi kwenye mishahara ya wafanyakazi wake ikilinganishwa na nchi nyingine wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki huku wafanyabiashara wakitozwa kodi kidogo.

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amesema pamoja na tozo kubwa ya kodi kwa mishahara ya wafanyakazi wa Tanzania ambayo ni asilimia 18, ikifuatiwa na Burundi inayotoza asilimia 10.3, Uganda inatoza asilimia 10.2, Kenya inatoza asilimia 6.8 huku nchi ya Rwanda ikitoza kodi kidogo zaidi kwa wafanyakazi wake ambayo ni asilimia 5.6.

Mbunge Kafulila ametoa kauli hiyo wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na kubainisha kuwa nchi ya Tanzania inaongoza kwa misamaha ya kodi kwa asilimia 4.5 ya pato la Taifa huku nchi nyingine za Afrika Mashariki zikitoa msamaha kwa kati ya asilimia 1 na 2.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!