Na GLADNESS MUSHI , Arusha
KAMPUNI ya Smile ya mawasiliano ya Smile imeweka mikakati ya kusaidia shule za Serikali ambazo zina maabara kwa kutoa huduma ya
mawasiliano(internet)bure itakayowawezesha wanafunzi waweze kusoma kwa kupitia mitandao.
KAMPUNI ya Smile ya mawasiliano ya Smile imeweka mikakati ya kusaidia shule za Serikali ambazo zina maabara kwa kutoa huduma ya
mawasiliano(internet)bure itakayowawezesha wanafunzi waweze kusoma kwa kupitia mitandao.
Hayo yameelezwa na Deo Ndejembe ambaye ni meneja kitengo cha mauzo katika kampuni hiyo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa mtandao wa smile kwa mkoa wa Arusha mapema leo.
Deo alisema kuwampango huo unalenga kuimarisha huduma za maabara katika shule za sekondari za serikali kwani wanafunzi wakiwa na huduma hizo wataweza kusoma na kwenda pamoja na soko la dunia ambalo linategemea zaidi huduma za mitandao.
Alidai kuwa mpango huo utaweza kuwanufaisha zaidi shule ambazo zina maabara pamoja na kompyuta hivyo basi hata kwa shule ambazo hazina maabara zinatakiwa kuweka mara moja ili ziweze kunufaika na mpango huo ambao umeshaanza
“Tunataka kuona kuwa lile lengo la serikali ambalo lililenga shule ziwe na maabara linatimia lakini pia maabara ziwe za kisasa zaidi na
ziweze kupata teknolojia ya mawasiliano bure kwani itasaidia hata ufaulu wa masomo kama sayansi kuweza kuongezeka’alisisitiza Deo
ziweze kupata teknolojia ya mawasiliano bure kwani itasaidia hata ufaulu wa masomo kama sayansi kuweza kuongezeka’alisisitiza Deo
Wakati huo huo alidai kuwa mpango huo wa kutoa huduma za Tekonlojia umeshaanza kwa shule 10 ndani ya Jiji la Dar es saalam lakini kwa mkoa wa Arusha shule ya Arusha School tayari imeshanufaika na mpango huo ambao ni bure
Naye Afisa mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)Innocent Mongi alidai kuwa bado mkoa wa arusha unahitaji huduma za mawasiliano zaidi kutokana na mwingiliano wa huduma kama vile uchumi, na utalii.
Mongi alidai kuwa uwepo wa mtandao huo wa Smile kwa mkoa wa arusha pia utachangia wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuweza kufanya biashra kutoka katika masoko mbalimbali duniani .
“Napenda kuwasihi wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa wanatumia vema mtandao huo ili kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo kwa mkoa wa arusha na kutokana na hili tunaamini kuwa Arusha itapata mabadiliko makubwa”alisema Mong
No comments:
Post a Comment