Mkutano wa Kumi na nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuanza leo mjini Dodoma ambapo Miswada ya sheria ya kura ya maoni na takwimu inatarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano huo utakaodumu kwa muda wa wiki tatu.
Mkurugenzi wa shughuli za Bunge JOHN JOEL amesema kutokuwepo kwa baadhi ya Wenyeviti wa Kamati za Bunge ambao ndiyo wajumbe wa kamati ya Uongozi kumechangia kutokamilika kwa ratiba rasmi hivyo baada ya kipindi cha maswali na majibu wajumbe hao watakutana tena.
Mkutano huo pia utajadili na kupitisha Miswada mbalimbali ya sheria ambayo haikufanyiwa kazi katika mkutano wa Bunge uliopita.

No comments:
Post a Comment