Saturday, 7 December 2013
LISSU AHOJI BUNGE KUTOAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MANDELA
Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), amehoji kwanini Bunge lilikuwa likiendelea na vikao licha ya kupata taarifa ya kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95) aliyefariki dunia juzi usiku.
“Ninaumwa sana, usiku kucha sikulala, nina homa, na hata sasa nimejikongoja tu kuja humu ndani, bado ninaumwa…nimeshangaa kuona msiba wa Bara zima, msiba wa Mtoto wa Afrika nadhani hatutapata mwingine kama yeye (Mandela), bunge linaendelea na vikao vyake kama kawaida…nilitegemea Bunge lingeahirisha kikao hiki walau kwa leo,” alisema.
Akijibu Spika wa Bunge ambaye mapema kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu na baada ya kumaliza kwa dua, alilitaarifa bunge kuhusu kifo cha Mzee Mandela, alisema, “mambo ya nchi yanaenda kwa utaratibu wa nchi.”
Lakini alisema kesho, Jumamosi, Bunge litatoa azimio la kumkumbuka na kumsifu.
“Tutatoa utaratibu wa kibunge kesho (leo), tutatoa azimio la kumkumbuka na kumsifu. Tunao utaratibu wa kuahirisha vikao vya Bunge lakini kwa hili ni utaratibu wa nchi,” alisema.
Hata hivyo, baada ya kumaliza kipindi cha wenyekiti wa kamati kuwasilisha taarifa za kamati zao, Spika aliwaomba wabunge kusimama kwa dakika moja kumkumbuka Mzee Mandela na kuiombea roho yake ipumzike mahali pema peponi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment