Tuesday, 26 November 2013

WATANZANIA WANAUTAMADUNI WA KUTOTAKA KULIPA KODI-MASALA


TRA

Hali katika eneo maarufu la biashara la Kariakoo jijini Dar es Salaam Tanzania imeendelea kuwa siyo ya kawaida baada ya wafanyabiashara kufunga maduka yao hapo jana kutokana na wafanyabiashara hao kugoma kutumia mashine za kieletroniki (EFD), ambazo wamelazimishwa kuzitumia ili kudhibiti ulipaji kodi nchini humo.
Akizungumza na  Sauti ya Amerika Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya mapato nchini Tanzania Bi .Diana Masala ambaye ameeleza pamoja na bei kubwa ya mashine hizo kuwa zina faida zaidi kwa wafanyabiashara na uchumi wa Tanzania kwa ujumla.
Amesema mashine hizo zimetengenezwa kulingana na mahitaji ya Tanzania  na unaingiza bidhaa zako zote ulizonunua ukiuza inajulikana kabisa umeuza kiasi gani na imebaki  kiasi gani tofauti na za mwanzo ambazo hazikuwapa matarajio waliyokuwa wakitegemea kwasababu zilitoa risiti tu na haikuweka kumbu kumbu yeyote, kwa hiyo hawakuweza kujua biashara inakwendaje na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Kuhusu kuelimisha wafanya biashara ameeleza kuwa walifanya kampeni na  waandishi wa habari, wafanya biashara wa sekta mbali mbali kama vile wafanyabiashara wa  spea za magari, ujenzi n.k.
Na pia walipita kila mahali jijini Dar es Salaam,  Ilala, Temeke na Kinondoni kwa kushirikiana na TCCIA  kutoa elimu hiyo.

Mahojiano na kaimu mkurugenzi wa TRA

 Aidha ameonngeza kuwa wametumia semina,  vipindi vya radio, vipeperushi  na taasisi kuzungumza na taasisi mbali mbali kama NBAA, TCCIA na nyinginezo  .
Amesema kuwa hii ni juhudi endelevu lakini kuna tatizo la watanzania kuwa na utamaduni wa kutokutaka  kulipa kodi , naye  mmoja wa wafanyabiashara waliogoma kufungua duka Kariakoo Bi. Saada Hussein alipozungumza na VOA ameeleza kuwa kugoma kwao kumetokana na bei kubwa ya mashine hizo ambazo wafanyabiashara wadogo na wakubwa ni vigumu kumiliki chombo hicho.
Mahojiano na mfanya biashara




Akijibu suala la kutokupenda kulipa kodi amesema wao wanalipa kodi kama kawaida  na risiti wanazo na TRA wanawakagua kila wakati ila suala ni kwamba uamuzi wa TRA si sahihi kwasababu watu wenye mtaji wanatofautiana mashine ni shilingi laki 8 za Tanzania na wameambiwa watakatwa asilimia 10 ya mauzo yao kila mwezi ili kuweza kuilipia , ameongeza kuwa wana malipo ya  kodi ya jengo, umeme, ulinzi  na  mwisho wa siku wanaona wananyonywa.
Kuhusu semina walizopewa na elimu anasema walielewa kuhusu bei za mashine lakini kwa sasa wameambiwa bei  imepunguzwa hadi laki 6 lakini si wafanyabiashara wote wanaoweza kumudu kununua mashine hizo .
Kuhusu mgomo wao amesema huenda ukaisha bada ya siku tatu lakini alikuwa hajaelewa vizuri makubaliano yao mpaka atakapofika kazini siku inayofuata.

CREDIT VOA.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!