Friday, 15 November 2013

WAHAMIAJI HARAMU 16 WAKAMATWA MAKONGO JUU JIJINI DSM




Watu 16 wanaosadikika kuwa wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia, waliokua  katika harakati za kusafirishwa kwenda Afrika kusini wametiwa mbaroni na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar-es-Salaam eneo la Makongo juu manispaa ya Kinondoni
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai kanda maalumu ya Dar-es-Salaam kamishina msaidizi wa polisi ACP Ahamedi Msangi amesema kuwa kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao, kunafuatia taarifa kutoka kwa wananchi wenye uzalendo, baada ya kutilia mashaka watu waliokuwa wamejifungia ndani nyumba iliyokuwa ikiendelea ujenzi.
Awali kamanda Msangi amesema kuwa wanamshikilia bwana Moshi Majungu anayedaiwa kuwa ni rafiki wa karibu na mchumba wa bwana Moshi Majungu, Bi Salome anayedaiwa na wahamiaji haramu kuwa ndiye bosi wao aliyekuwa akiwahudumia kwa chakula, ambapo kamera ya ITV imeshuhudia matandiko na chupa za mkojo na kinyesi katika jengo hilo.
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida kamera ya ITV ilishuhudia Kibanda cha kufugia kuku cha jirani na bwana Moshi Majungu, alichokuwa amejificha mtuhumiwa huyo, baada ya jaribio lake la kutaka kuwakimbia polisi waliokuwa wameweka mtego ili kumkamata, nao baadhi ya wananchi na mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo,bwana saidi Makilikiti wamesema kuwa bwana Moshi Majungu amekuwa na tuhuma za kiutapeli katika mtaa wao na kuwa ana kesi katika vituo vya polisi jijini

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!