Stori: Gladness Mallya
SEXY lady wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesheherekea mwaka mmoja na wenzake tangu alipoacha kutumia madawa ya kulevya ‘unga’.
SEXY lady wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesheherekea mwaka mmoja na wenzake tangu alipoacha kutumia madawa ya kulevya ‘unga’.
Wikiendi iliyopita Ray C alitupia picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram zilizomuonesha akiwa na wenzake katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar ambako huwa wanapata dozi ya madawa ya kulevya.
Aliandika: “Nawapenda sana hawa wenzangu wote, tuligundua tatizo tukasaidiwa na sasa tumepona na tunamshukuru Mungu...Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana.”
Baada ya kuandika maneno hayo wadau mbalimbali walimpongeza Ray C na kuwataka wengine wanaotumia madawa ya kulevya kufuata nyayo zake.
No comments:
Post a Comment