Thursday 28 November 2013

RAIS KIKWETE ATANGAZA KUANZA KWA UJENZI WA KIMATAIFAWA RELI YA KATI

Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mara moja mpango mkubwa wa ujenzi wa kimataifa wa reli ya kati baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara kwa kiwango cha lami nchini kote. 




Mh rais kikwete ametangaza mpango huo mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa,wakati akihutumia maelfu ya wananchi wa mji wa Old Maswa wilayani Bariadi mkoani Simiyu muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa barabara ya kilometa  71.7 inayojengwa na kampuni ya cc ya nchini China kwa kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 70.

Hata hivyo rais Kikwete,amesema serikali,imekuwa ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara yakiwemo madaraja ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, huku akisema kati ya madaraja makubwa matano yalipangwa kujengwa baada ya uhuru,rais wa kwanza Mwl Julius Nyerere ameweza kujenga daraja la Kirumi mkoani Mara na rais  wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa amejenga daraja la mto Rufiji na sasa serikali yake imekamilisha ujenzi  wa madaraja matatu yaliosalia.

Awali waziri wa ujenzi  Mh. John Pombe Magufuli,akimkaribisha rais Kikwete kuzungumza na wananchi ambao wamejitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe hilo la msingi,amesema ujenzi wa barabara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa kuunganishwa na mikoa ya Mwanza na mara pamoja na nchi jirani ya Kenya,huku mtendaji mkuu wa wakala wa barabara mhandisi Patrick Mfugale,akitoa kilio kwa rais kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kulipa wakandarasi nchini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!