Mtoto Omar Said
Katika hali Isiyo ya kawaida, wala kufikirika Baba mmoja aliyekuwa akiishi na binti mmoja jina Hamida, na mtoto wake mmoja Omar Said , alijikuta akichukua kiberiti na mafuta na kumchoma Binti huyo kama karatasi. Kisa kizima hichi hapa mtoto akisimulia:
"Tulikuwa tumelala usiku mimi na mama tu chumbani, kwani ilikuwa ni kawaida baba kuchelewa kurudi na mara nyingi huwa anarudi akiwa amelewa na kumpiga mama kila siku , mama anapiga kelele usiku mpaka baba mdogo anayeishi jirani huja na kuingilia ugomvi" Mtoto akiendelea kusimulia akiwa anabubujikwa na machozi:
"Siku hiyo baba alirudi usiku sana akiwa amelewa kama kawaida yake akamuamsha mama, halafu nikamsikia anamuambia mama kwenu siendi na kama utaendelea kunilazimisha nitoe mahali basi leo ndio mwisho wako, nikasikia tu mama amepiga kelele kubwa ambayo sio ya kawaida, mara nikaona kama moto mkubwa ndani nikaamka na mimi nikaanza kupiga kelele nilipo angalia vizuri nikaona kumbe ni mama yangu anateketea na moto niliendelea kupiga kelele lakini mama yangu wakati huo alikuwa ameshanyamaza haoengei tena, siku hiyo sijamuona hata baba mdogo kuja kuamualia, baba alikimbia sikumuona tena hadi leo"
SOURCE PAPARAZI BLOG
No comments:
Post a Comment