Sunday, 10 November 2013

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema hautahusika na malipo ya matibabu kwa wanachama wao watakaoathirika na utumiaji wa dawa za kuongeza maumbile.(HD)

article-2265277-17117548000005DC-778 306x423 a9381
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema hautahusika na malipo ya matibabu kwa wanachama wao watakaoathirika na utumiaji wa dawa za kuongeza maumbile.(HD) 

Akizungumza kwenye kongamano la wadau wa mfuko huo mkoani hapa hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini alisema mfuko hautatoa huduma kwa mwanachama aliyeathirika na dawa za kuongeza maumbile ambazo zimepigwa marufuku na Serikali.

Dk Fikirini alisema mfuko huo unatoa huduma ya matibabu kwa wanachama wake, ila hauhusiki na waathirika wa dawa zilizopigwa marufuku na Serikali ikiwamo za kuongeza maumbile maarufu kama dawa za Kichina.
 
"Leo tupo hapa pamoja ili kuzungumza nanyi wanachama wetu, kujadili na kuona jinsi tunavyoweza kuuboresha mfuko, ila napenda kusema NHIF hautamtibu mwathirika wa dawa za kuongeza maumbile," alisema Dk Fikirini.

Aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na madiwani, kuwashawishi wajawazito kujiunga na mradi wa kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua (KFW), ambao umekuwa mkombozi kwa baadhi ya maeneo. Dk Fikirini alisema mradi huo umekuwa ukiwanufaisha wajawazito kujifungua salama baada ya kupata ushauri na matibabu wakati wa kliniki, hivyo wanawake wengi hawana taarifa na mradi huo.

Awali, Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga, Ali Makababu alisema wananchi wengi hawana mwamko wa kujiunga, hivyo kutaka elimu itolewe shuleni, vyuoni na kupitia matangazo ya televisheni.

Alisema hatua hiyo imesababisha kuongezeka kwa makali ya maisha.

CHANZO MWANANCHI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!