Maulidi ya kumuombea marehemu Sharo Milionea imekamilika, kisomo kisomwa nyumbani kwao asubuhi ya November 26 2013 kisha wote kuelekea makaburini ambapo kulikua na dua pia ikiwa ni mwaka mmoja kamili umetimia toka Sharo afariki ambapo kifo hiki kilitokana na ajali aliyoipata Maguzoni Muheza nje kidogo ya jiji la Tanga alipokua anaelekea nyumbani kwao Lusanga.
Yafuatayo ni mambo machache yaliyozungumzwa na Mama mzazi wa Marehemu pamoja na rafiki yake Sharo (Kitale), waelikua marafiki sana na hata walishirikiana kwenye kazi ya sanaa ya kuigiza na muziki pia.
1.Mama mzazi anasema huwa anaumia sana anapomkumbuka mwanae, ni taarifa za ghafla alizipata usiku wa siku ya tukio akiwa amelala ambapo kwa asilimia zote alikua anamtegemea Sharo Milionea kumsaidia kimaisha.
2. Mama amekua akiumia sana kukuta kalenda zenye picha ya Marehemu majumbani mwa watu, kalenda ambazo zimekua zikiuzwa kote Tanzania bila idhini ya Familia na haijulikani nani amezitengeneza.
3. Mama anasema hakuna makubaliano yoyote aliyoletewa au kuambiwa kuhusu mali au kazi za kisanaa alizoziacha Marehemu wala hajapewa malipo yoyote ya Marehemu.
4. Kitale anasema ‘movie ya mwisho aliyocheza na Sharo Milionea ‘IMPOSSIBLE’ ipo mikononi mwake sasa hivi na bado haijatoka, imechelewa kwa sababu ya usumbufu alioupata kutoka kwa Maproducer aliowakabidhi na pia kufutika baada ya kufanyiwa editing’
5. ‘Tukizungumzia mauzo ya nyimbo za Sharo zinazotumika kama milio kwenye simu mpaka sasa ni kwamba Sharo alikua ameingi mkataba na watu lakini mama yake kathibitisha hakuna chochote alicholipwa kutokana na hiyo kazi, bado sijajua utaratibu unaoendelea kuna uwezekano labda akaja akapewa’ – Kitale
6. ‘Binafsi sijafanya muziki tangu marehemu Sharo Milionea afariki, labda kuanzia sasa hivi ndo nitakuwa tayari kutoa wimbo na shughuli zangu nyingine,tulikua tumepanga mashambulizi makubwa na tulikua tunakuja kuwashika’ – Kitale
7. Kitale na Mama Mzazi walifatilia Account ya benki iliyokua ya Sharo Milionea ili kujua kama kuna pesa yoyote imebaki, walifanikiwa kuipata Account lakini hakuna pesa yoyote waliyoikuta.
No comments:
Post a Comment