UMEKUWA ni kama wimbo wa taifa unaoimbwa kwa ajili ya wasanii wa kike Tanzania, kutokana na kurudiwa
kwa maneno hayo hayo kila kunapokucha.
Serikali na baadhi ya mashirikisho husika ya sanaa yamekuwa yakikemea suala la wasanii wa kike
kuvaa nguo za nusu uchi katika maonesho yao, lakini kwa asilimia kubwa hakuna linalorekebishwa.
Sitaki kuamini kama msanii anapovaa nguo za aina hiyo ndiyo anaimba vizuri au anacheza vizuri
tofauti na akivaa nguo za kumstiri mwili wake.
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa, aliutaka uongoz
i wa Shirikisho la Muziki Tanzania, umchukulie hatua za kinidhamu msanii wa muziki wa mduara,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kwa kosa la kuvaa nguo ambazo hazikustahili kuvaliwa kwenye umati wa watu
No comments:
Post a Comment