Tuesday, 8 October 2013

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU UCHANGIAJI WA MAENDELEO


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano a Kimataifa, Mhe. Mahadhi J. Maalim (Mb.) akisikiliza kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu kuchangia Maendeleo uliofanyika Mjini New York, Marekani tarehe 7 Oktoba, 2013. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Bw. Ali Mwadini, Katibu wa Naibu Waziri.




Mhe. Maalim akitoa hotuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Kuchangia Maendeleo (Financing for Development) uliofanyika Mjini New York, Marekani tarehe 7 Oktoba, 2013. Katika hotuba yake Mhe. Maalim alisema kuwa Tanzania inaendelea kupiga hatua katika maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza jitihada katika ukusanyaji kodi na kuzingatia utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na utawala bora.


Balozi Mushy, Bw. Mwadini pamoja na Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York wakifuatilia hotuba hiyo kwa makini.

Habari kwa hisani ya Michuzi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!