Wilbert Moland na Khatimu Naheka
UONGOZI wa Yanga umefanya kikao cha siri katika kuamua wapi wataificha timu yao kabla ya kuumana na Simba, lakini wakapata jibu moja kwamba kisiwani Pemba ndiyo sehemu muafaka.
Taarifa ambazo zimelifikia Championi Ijumaa, zinasema uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake, Yusuf Manji, umekubaliana kwa pamoja kwamba wakakifiche kikosi chao hicho Pemba, sehemu ambayo waliweka kambi msimu uliopita, kabla ya kucheza na Simba katika mchezo wa marudiano, uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Chanzo hicho kutoka ndani ya Yanga kimeleeza kuwa, kabla ya maamuzi hayo, awali Yanga walikubaliana kuwa kikosi chao hicho kitaweka kambi jijini Mwanza ambako wangecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda, ratiba ambayo ilivunjwa ghafla, huku sababu zikiwa siri nzito.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, mara baada ya Yanga kumaliza mchezo wao wa kesho dhidi ya Kagera Sugar, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, kikosi hicho kitarejea jijini Dar, siku ya Jumapili kwa ndege na kuondoka Jumatatu kwenda kisiwani humo.
“Tulishakubaliana kuwa timu itabaki Mwanza kwa kambi, lakini tumekutana tena jana (juzi) katika kikao kingine na kuvunja ratiba hiyo, siwezi kukwambia sababu, hiyo ni siri yetu, lakini sasa tutaweka kambi Pemba, tutarudi Dar siku chache kabla ya mechi,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Sasa hivi tunaelekeza nguvu zetu katika mchezo dhidi ya Kagera, tunataka kuhakikisha tunashinda ili tukiingia katika maandalizi ya Simba tuwe na morali ya hali ya juu.”
GPL.

No comments:
Post a Comment