Sunday, 13 October 2013

PINDA ACHANGIA SHILINGI 10,000,000 KAMPENI YA KANSA YA MATITI

 

 Baadhi ya Waandamanaji wakiwa wamebeba bango la kuhamasisha vita ya Kansa ya Matiti kwa Wanawake nchini.
  Dk.Hussein Mwinyi (Katikati mwenye saa nyeusi mkononi) akiongoza  waandamaji kutoka maeneo ya Mbezi Jogoo kuelekea Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar.
  Dk. Hussein Mwinyi (wa pili kutoka kulia) akiongoza waandamanaji mapema leo mchana kutoka Mbezi Jogoo kuelekea Kunduchi Hotel.
Baadhi ya Wazungu walioshiriki maandamano hayo.
Baada ya safari hiyo wakiwa wanapumuzika ,huku  Msanii mkongwe wa Bongo move Jackobo Steven maarufu kama ‘JB’akinywa  maji.
Msanii wa Bongo freva maarufu kama Lulu katikati .
Watoto nao hawakuwa nyuma nao walikuwepo.
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Hussein Mwinyi  leo ameongoza maelfu ya waandamanaji katika maandamano ya amani ya kupiga vita kansa ya matiti kwa wanawake nchini na kutoa mchango wa shilingi 10,000,000 kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 Dk.Mwinyi ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu,  Mizengo Pinda  kwenye  harambee hiyo ya kusaidia udhibiti wa kansa ya wanawake nchini iliyoendeshwa na Taasisi ya Kudhibiti Kansa ‘ORCI’ chini ya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar iliyofanyika  leo katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar  na kuhudhuriwa na waandamanaji mbalimbali nchini, akisoma hotuba ya Mhe. Pinda.
 “Waziri mkuu anaungana na Taasisi ya Kansa nchini ‘ORCI’ hiyo japo hakufika na amechangia shilingi milioni 10, na amewataka wanawake nchini kuchukua tahadhari mapema juu ya tatizo la kansa ya matiti, hii ni pamoja na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara juu ya Afya zao,”  alisema Dk Mwinyi.
 Hata hivyo Mkuu wa shughuli hiyo Dr.Julius Mwaiselage amesema  anapongeza mwamko na hamasa kubwa aliyoutoa Staa wa sinema za kibongo Jackob Steven ‘JB’ kwa kuchangia Shilingi Milioni 2.
Wadau wameombwa kuchangia  Mfuko wa Hospitali ya Ocean Road kwa M-PESA namba Namba 175555.
(NA JELARD LUCAS GLP

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!