BG
Group leo imetanganza kukamilisha kikamilifu majaribio ya uchimbaji kwenye eneo
la gesi la Pweza ndani ya bahari kusini
mwa Tanzania, na kuhitimisha programu kubwa ya kufanya tathmini kwenye Kitalu namba 4.
Hii inathibitishamatarajio ya ubora katika hifadhi hii ya gesi asilia
na kufanya maendeleo chanya.
Hifadhi
ya gesi ya Pweza inakadiriwa kuwa kilometa 70 kutoka kwenye pwani ya Tanzania kwenye
kina cha maji cha meta1 400 .
Matokeo ya awali kutoka kwenye majaribio ya
uchimbaji wa gesi kwenye kitalu namba 3 cha Pweza yamethibitisha kuwepo na
hifadhi ya gesi yenye ubora wa hali juu,.Majaribio ya uchimbaji ni utaratibu
unaokubalika katika shughuli za utafutaji wa gesi, na ni utaratibu unaotumika katika kubaini
ubora wa hifadhi ya gesi.
Majaribio
matatu yalifanyika katika hifadhi ya gesi ya Pweza , jaribio la kwanza
lilifanyika kwenye Kitalu namba 4, ambapo
mtiririko wa gesi ulikuwa katika kiwango cha futi za ujazo
milioni 57 cha gesi kwa siku, kulingana na uwezo wa mwisho wa kifaa
kilichotumika katika majaribio ya uchimbaji.
Muhimu zaidi, majaribio haya yameonyesha
kwambavisima vitakavyochimbwa kwa uzalishaji vinaweza kutiririka gesi kwa kiwango cha juu
na kwamba hifadhi ya gesi ya Pweza kimsingiina uzalishaji mkubwa kulinganisha
na visima vingine vilivyochimbwa na
kampuni ya BG Tanzania.
Rais
na Meneja Mkuu wa kampuni ya BG Afrika Mashariki, Derek Hudson,alisema: “Tumefurahishwa
na matokeo ya majaribio yetu na tathmini katika Kitalu namba 4 cha gesi;kuna
raslimali za gesi za futi za ujazo wa trilioni4
(tcf). Kazi iliyofanyika inaonyesha gesi yenye ubora wa hali ya juu
kwenye maeneo hayana tunaendelea kushirikiana na washirika wetu Serikalini na
katika sekta binafsi kuhusu matarajio ya kuweka mtambo wa Gesi Asilia (LNG) , ambapo
uzalishaji kutoka kwenye vitalu hivi vya gesi utakuwa ukitegemea mtambo huu.”
Majaribio haya
katika kisima cha Pweza pia yamethibitisha rasilimali ya gesi ambapo kampuni ya
BG hivi karibuni imetangaza kuwa na raslimali za jumla za gesi nchini Tanzania
zinazofikia futi za ujazo trilioni13.
Meli ya uchimbaji katika kina kirefu iliyokodiwa na kampuni ya BGiitwayo
Deep SeaMetro-1kwa sasa imehamia upande wa kusini katika Kitalu namba 1 ambapo inafanya
uchimbaji wa tathmini (appraisal) kwenye eneo jingine ilipogunduliwa gesi liitwalo
Mzia.
BG Group kama mwendeshaji ina
asilimia 60 ya hisa katika Vitalu namba 1, 3 na namba 4 ndani ya bahari nchini Tanzania, ambapo Ophir Energy ina hisa ya asilimia 40. Washirika kwa sasa wanazifanyia tathmini
data za 3-D za seismikiili kusaidia
kubaini maeneo lengwa ndani ya bahari kwa ajili ya programu mpya ya utafutaji
wa gesi mwaka 2014
No comments:
Post a Comment