Hofu ya usalama imeendelea kutanda Mjini Mombasa nchini Kenya
kufuatia watu wenye silaha kumuua Kiongozi maarufu wa Dini ya Kiislam
Sheikh Ibrahim Ismail pamoja na wafuasi wake wanne walipokuwa wanarejea
nyumbani wakitoka Msikitini. Sheikh Ismail ambaye alikuwa mrithi wa
Abdoud Rogo Mohammed amekuwa akitajwa kuwa msambazaji wa itikadi za
Kundi la Wanamgambo la Al Shabab la nchini Somalia linalotajwa
kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga nchini Kenya.
Kiongozi huyo wa kidini ambaye alikuwa anaongoza Msikiti wa
Musa unaotajwa kuwa na itikadi kali amekuwa akitoa mahubiri yanayotajwa
kuchochea wananchi wengi nchini Kenya kujiunga na Kundi la Al Shabab.
Sheikh Ismail ameuawa kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Sheikh Rogo
aliyeuawa akituhumiwa kuwa Msemaji wa Kundi la Al Shabab nchini Kenya
na aliuawa mwezi Agosti mwaka 2012.
Jeshi la Polisi limethibitsha Sheikh Ismail akiwa na wenzake wanne
walishambuliwa na watu wenye silaha wakiwa kwenye gari lao na kupoteza
maisha kisha watu hao wakatokokea kusikojulikana.
Polisi wameendelea kusema mwili wa Sheikh Ismail ulikutwa umejawa na
damu kutokana na mashambulizi ya risasi yaliyofanywa na watu hao
waliokua wamejihami vilivyo kwa silaha nzito.
Wafuasi wa Sheikh Ismail wamejitokeza na kulituhumu Jeshi la Kenya
kuhusika kwenye mauaji ya Kiongozi wao tuhuma zilizokanusha vikali na
Jeshi la Polisi linaodai hajahusika kwa namna yoyote.
Hofu imeanza kuzagaa huenda kukafanyika maandamano makubwa kwenye Mji
wa Mombasa mchana wa leo kuonesha hasira za wafausi wa Sheikh Ismail
kufuatia kifo cha Kiongozi wao wa Kidini.
Sheikh Ismail amekuwa mstari wa mbele kuhubiri siasa za Kundi la
Wanamgambo la Al Shabab huko Mombasa na kuwashawsihi vijana wengi kuwa
tayari kujiunga na kundi hilo linalotajwa kuwa kitisho cha usalama
nchini Kenya.
Mtangulizi wake Sheikh Rogo wakati wa uhai wake alikuwa miongoni mwa
watu waliokuwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Marekani
pamoja na Umoja wa Mataifa UN.
Kundi la Wanamgambo la Al Shabab limeendelea kuwa hatari baada ya
kjutekeleza shambulizi lililochangia vifo vya watu sitini na saba baada
ya kuliteka Jumba la Biashara la Westgate.
No comments:
Post a Comment