Thursday, 10 October 2013
JAMANI HII YA KUCHUKUA SHERIA MIKONONI MWETU NI HAKI? HUNA HAKI YA KUMMUA BINADAMU MWENZIO, HII INASIKITISHA KWAMBA TUMEFIKIA HAPA?
Hili swala la kuchukulia sheria mkononi linatisha jamani, hata watu wanashauriwa wakimgonga mtu barabarani ni bora wakimbilie polisi, hata watu wenye nia njema tu hushindwa kusimama kwa kuhofia maisha yao na kuogopa mob justice.
Tabia ya kujichukulia sheria mkononi imekuwa ni tatizo kubwa nchini na ni kinyume na haki za binadamu. Hebu tazama picha hii wananchi wakijichukulia sheria mkononi kwa mtu anayedhaniwa kuwa ni mwizi, Je, mtu
akiamua kumpakazia mtu kumwita mwizi kwa sababu zake binafsi na watu wakachukua hatua kama hii kwa mtu asiyekuwa na hatia?
MIMI BINAFSI NAKEMEA TABIA HII NA KWA KWELI HIVI KWELI TUMEFIKIA HAPA? NA HAWA WANAOSHANGILIA PEMBENI JAMANI KUNA VYOMBO VYA SHERIA ACHENI HII ROHO YA UNYAMA, HUU NI UUWAJI!
toa maoni yako jinsi gani tunaweza kukomesha hii tabia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment