Mfanyakazi wa kazi za ndani ‘hausigeli’ aliyetajwa kwa jina moja la Anna (14) amedai kubakwa na baba ambaye ni bosi wake aliyetambuliwa kwa jina moja la Andrea.
.Kwa mujibu wa hausigeli huyo, alifika katika nyumba hiyo mwaka jana mwezi wa kumi na moja baada ya kuchukuliwa nyumbani kwao, Morogoro na mama ambaye ni mke wa mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la mama Nimpa.
Alisema kuwa baada ya kufika katika nyumba hiyo, alikuwa akifanya kazi kama kawaida huku akidai kuteswa na mama huyo kwa kumpiga na mpaka sasa hakuwahi kumlipa mshahara wake hata wa mwezi mmoja.
Alidai kuwa baada ya kuona mateso yamezidi, hivi karibuni aliamua kukimbia nyumbani hapo na kwenda katika serikali za mitaa kuomba msaada ambapo viongozi walimsaidia kumhifadhi na kuwatumia mabosi zake barua ya wito.
Baada ya kutumiwa barua, mabosi hao walifika katika ofisi hizo na kukutana na viongozi ambapo mazungumzo yalianza kuhusu mshahara wake.
Katika kikao hicho, bosi wake (mama Nimpa) alikiri kuwa ni kweli anadaiwa na msichana huyo na walielewana na mama yake kuwa mshahara wake kwa mwezi ni elfu ishirini lakini alipofika Dar, kazi zote akawa anafanya mwenyewe, jambo lililosababisha amtaarifu mama yake kuwa atamlipa elfu kumi na tano maana kazi haziwezi hivyo walikubaliana na kuendelea na maisha.
Katika kikao hicho kizito kilichofanyika katika ofisi hizo za serikali za mitaa, hausigeli huyo alidai kwa mdomo wake kuwa bosi wake huyo wa kiume aliwahi kumbaka na kipindi hicho walikuwa na dada yake (dada wa bosi) ambaye naye alipewa mimba na kaka yake huyo ambaye ni bosi wa msichana huyo.
Baada ya hausigeli huyo kutoa siri hiyo, mama Nimpa aliangua kilio kama mtoto mdogo mbele za watu waliokuwa kwenye kikao hicho huku akilaumu na kusema kuwa huo ni mpango umesukwa na majirani ambao wamemfundisha hausigeli huyo ili kumchafulia mumewe jina kama ilivyokuwa kwenye tukio la wifi yake.
Kutokana na mateso hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo, Demetrius Mapesi alifikia uamuzi kuwa hausigeli huyo anatakiwa kulipwa fedha zake za miezi kumi na moja kisha arejee kwao Morogoro.
Mabosi hao walikubaliana na uamuzi huo na kwa kuanzia walitoa Sh. laki moja na ishirini wakiahidi kumalizia fedha nyingine siku iliyofuata huku mwanaume huyo aliyetuhumiwa akiinamisha kichwa na kusikitika kwa aibu
No comments:
Post a Comment