Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt na mke wake walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano aliowapa katika kipindi chao cha ubalozi hapa nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga mke wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano aliowapa katika kipindi chao cha ubalozi hapa nchini. Mama Salma Kikwete alikuwepo pia katika kuwaaga wanadiplomasia hao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe. Alfonso Lenhardt leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru.
(PICHA NA IKULU)

---
Tanzania na Marekani zimeimarisha mahusiano yao katika kipindi cha miaka minne iliyopita kutokana na uhusiano na ushirikiano mzuri wa balozi anaemaliza muda wake nchini Mh. Alfonso Lenhardt.
“Asante kwa kazi nzuri uliyoifanya katika kipindi chote cha miaka minne uliyoitumikia hapa Tanzania. Mambo mengi na makubwa yenye kuleta maendeleo na manufaa kwa Tanzania yamefanyika hapa nchini na umeyasimamia na kuyafanikisha ipasavyo”.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemueleza Balozi Lenhardt leo alipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa nchini.
Rais Kikwete amesema ushirikiano wa nchi hizi mbili umekua na kuimarika zaidi na anatarajia kuwa balozi ajaye naye atakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza na kuimarisha zaidi mahusiano baina ya nchi hizi.
Naye balozi Lenhart amesema Tanzania iko moyoni mwake na ataendelea kuwa balozi wa Tanzania popote alipo.
“Nikushukuru wewe mheshimiwa Rais na serikali yako kwa ushirikiano mzuri na utayari wa kunisikiliza na kunisaidia wakati wote nilipohitaji ushauri wako, umekuwa msaada mkubwa kwangu. Asante kwa ushirikiano wako na siku zote nitaendelea kuwa balozi wa Tanzania kwani Tanzania iko moyoni mwangu”.
Imetolewa na;Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
Dar es Salaam.
07 October, 2013
No comments:
Post a Comment