Tuesday, 10 September 2013

ZANZIBAR YAAPA KUISHITAKI MELI ILIYOKAMATWA NA TANI 30 ZA BANGI ITALIA



Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itafungua mashtaka dhidi ya kampuni ya Gold Star, baada ya meli yake kukamatwa na tani 30 Za mihadarati aina ya bangi Kisiwa cha Malta Vessel, nchini Italia.


Hatua hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi wa Mamalaka ya Usafiri Baharini (ZMA), Abdi Omar Maalim, alipozungumza ofisini kwake Mlandege Zanzibar, jana.


Maalim alisema kwa mujbu wa sheria namba 5 ya mwaka 2006 ya usafiri baharini, kampuni hiyo imekiuka masharti ya usajili, ambayo yanazuia meli kubeba silaha, dawa za kulevya, wakimbizi au mzigo wowote wenye biashara haramu.


Alisema wanasheria wa ZMA wataipitia sheria hiyo kabla ya kuamua kuishtaki kampuni hiyo mabaharia tisa wanaodaiwa kula njma za kusafirisha bangi, kabla ya kukamatwa huko Italia.


“Tunategemea kufungua mashtaka dhidi ya Kampuni ya Gold Star kwa kukiuka masharti ya fomu ya usajili, ambayo yanazuia meli kubeba mihadarati, silaha, wakimbizi au mzigo wowote haramu,” alisema Maalim

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!