Wednesday, 11 September 2013

WAZIRI MKUU ATAKA CHINA IJENGE VIWANDA NCHINI, NIA NI KULETA UWIANO WA KIBIASHARA ASEMA PINDA..



picha no.6WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema uwiano wa kibiashara baina ya Tanzania na China hauko sawa kwa sababu Tanzania inauza nchini China bidhaa ambazo hazijasindikwa lakini inanunua kutoka huko bidhaa ambazo zimekamilika (finished products).
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Septemba 10, 2013) wakati akifungua maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni za Kichina kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Maonyesho hayo yanayotarajiwa kufungwa Ijumaa, Septemba 13, mwaka huu, yanahudhuriwa makampuni zaidi ya 200 kutoka majimbo 14 ya China

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!