.
Watuhumiwa wa madawa ya kulevya wakiwa wameficha nyuso zao katika Mahakama Kuu jijini Dar leo.
Mmoja wa watuhumiwa akiwa ameinamisha kichwa chake kukwepa kamera za wanahabari. Askari Magereza akimtia pingu mtuhumiwa katika kesi ya madawa ya kulevya. Watuhumiwa wakificha sura zao kwa wanahabari waliokuwa na hamu ya kupata picha zao.
HALI ya sintofahamu imetokea leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania
jijini Dar es Salaam wakati Jaji Mwakipesile alipomaliza kusikiliza kesi
inayowakabili watuhumiwa wa madawa ya kulevya. Waandishi wa habari
waliwakaribia watuhumiwa hao ili kuwapiga picha ndipo walipowakwida
baadhi yao na wengine wakiwa 'busy' kuficha nyuso zao kwa kile
walichodai kutotaka kupigwa picha wala kutolewa kwenye vyombo vya
habari. Aidha baadhi yao walitinga kortini wakiwa wamevalia 'Ki-ninja'
(wakiwa wameficha sura zao zisifotolewe) hali iliyozua mtafaruku kortini
hapo, kabla ya polisi kuwapiga pingu kuwarudisha rumande. Baada ya jaji
kuahirisha kesi hiyo, baadhi ya watuhumiwa walikuwa mbogo huku mmoja
wao akimtupia teke mpigapicha hali iliyoonesha hakutaka kabisa
kuchukuliwa picha na waandis