VYAMA vya upinzani nchini, vimeamua kuungana ili kunusuru mchakato wa Katiba mpya. Msimamo huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam, wakati wenyeviti wa vyama hivyo ngazi ya taifa, walipofanya mkutano na waandishi wa habari.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, aliyesoma tamko lao ni Profesa Lipumba, ambaye alisema ushirikiano wao umelenga kuhakikisha Katiba mpya inapatikana kwa maslahi ya Watanzania.
Alisema kwamba, ushirikiano huo umetokana na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kupitishwa bungeni Septemba 6, mwaka huu, kwa nguvu na wabunge wa CCM.
Alisema kuwa, muswada huo ulipitishwa ukiwa na kasoro mbalimbali, zikiwamo za CCM kuingiza vipengele bila kufuata utaratibu kwa maslahi yao na pia wananchi wa Zanzibar hawakushirikishwa ipasavyo













No comments:
Post a Comment