Saturday, 14 September 2013

UWOYA MBARONI KWA WIZI WA SIMU!

 

Na Waandishi Wetu
MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
MAMBO yanaendelea kumwendea kombo mwigizaji huyo huku akiwa ameanza kuporomoka vibaya kwenye sanaa na kujikuta akiingia  matatani kwa tuhuma za aibu.
HABARI ZA KIPOLISI
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo  ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya.
MMILIKI AMWANIKA UWOYA
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi, Mohammed alisema simu hiyo aliinunua mwaka huu kwenye Duka la Grande Center jijini New York, Marekani alikokwenda kwa shughuli zake.Akasema Agosti 22, mwaka huu alirejea Bongo akiwa na simu hiyo ambayo ni toleo jipya la mwaka huu.
“Nilirejea hapa nchini nikiwa na simu hiyo. Tena unajua simu yenyewe ni ya kisasa, toleo la mwaka huu,” alisema Mohammed.Alisema Agosti 23, mwaka huu, akiwa kwenye gari katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Nyamwezi, Kariakoo, Dar aliibiwa simu hiyo na mtu asiyemtambua.
“Nilikwenda Polisi Msimbazi kuandikisha maelezo na kupewa RB hiyo. Lakini nilitumia njia ya kitaalam kufuatilia, nikagundua simu yangu inatumiwa na mtu anayeitwa Peter, nikampigia simu kumwambia lakini hakuweka wazi aliipataje?
Mohammed alisema baada ya dakika kumi, alipigiwa simu na Uwoya na kumchimba mkwara kuhusu simu hiyo huku akisema ni yake yeye, jambo ambalo lilimshangaza jamaa huyo.
“Nilirudi Msimbazi na kuwaambia ndipo polisi wakaanza kazi ya kumsaka ili wamkamate. Leo (Alhamisi) amekamatwa akiwa na hiyo simu yangu,” alisema.
Irene Uwoya.
UWOYA AULIZWA ALIKOIPATA SIMU HIYO
Inadaiwa kuwa polisi walimuuliza Uwoya alikoipata simu hiyo ambapo alisema alipewa na jamaa yake wa Afrika Kusini huku mlalamikaji huyo akitoa risiti ya kununulia.
AONDOLEWA POLISI KWA MLANGO WA NYUMA
Baada ya kumaliza kuhojiwa kituoni hapo, Uwoya alitolewa kinyemela kwa mlango wa nyuma ili mapaparazi waliopiga kambi nje ya kituo hicho wasimfotoe.

GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!