KIFO cha aliyekuwa msanii wa Bongo Movies, Zuhura Maftah ‘Malisa’ kimeacha simanzi kwa wengi lakini kwa mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ni zaidi kwani alimwaga chozi lililoibua minong’ono kuwa lina kitu cha ziada nyuma yake, Ijumaa lina tukio kamili.
Haukupita muda mrefu ambapo mwili wa Malisa ulipoanza kuagwa lakini Steve hakuonekana hadi alipotokea akiwa wa mwisho akisaidiwa na baunsa ili asidondoke.
Baadaye aliingiza mikono kwenye jeneza kisha akashika mwili wa Malisa akakiinua kichwa na kumbusu marehemu mdomoni kwa dakika kadhaa.
Steve aliendelea kuling’ang’ania jeneza hilo huku akilia, jambo lililoibua minong’ono mingi kuwa machozi yake yalikuwa na kitu cha ziada nyuma yake kwa sababu ilikuwa ni zaidi ya kilio.
“Maskini Steve, anaonekana ameuamia kuliko mtu yeyote. Ukweli ni kwamba alimpenda sana marehemu. Kwa vyovyote machozi yake yana kitu cha ziada, siyo bure. Labda aamini kama Malisa hatunaye,” alisema mmoja wa wasanii wa Bongo Movies.
Alipofikishwa makaburini, wakati wa zoezi la kurudishia udongo kaburini, Steve alishindwa tena kujizuia, aliendelea kumwaga machozi huku akizungumza vitu visivyoeleweka zaidi ya kusikika maneno ‘wasanii wa Bongo Movie’.Hata hivyo, gazeti hili lilipotaka kujua kulikoni akamwaga chozi kiasi hicho, Steven hakuwa na ‘mudi’ ya kuzungumza chochote.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Steve na Malisa walikuwa watu wa karibu, hivyo inawezekana ndiyo sababu ya mwigizaji huyo kumwaga machozi kuliko wengine na kufuatiwa na Yvone-Chery Ngatwika ‘Monalisa’ na waigizaji wengine.
Kwa upande wa filamu, kabla ya mauti, Malisa alionekana kwenye Filamu ya Big Dady ya marehemu Steven Kanumba ambaye naye alizikwa kwenye makaburi hayo ya Kinondoni
CHANZO. GPL
No comments:
Post a Comment