›Serikali imesema itatumia gharama yoyote kwa ajili ya kuhifadhi Ikolojia ya bonde la mto Mara
Serikali imesema itatumia gharama yoyote kwa ajili ya kuhifadhi Ikolojia ya bonde la mto Mara huku ikisema itatii itifaki ya pamoja ya makubaliano kati ya Kenya na Tanzania katika kulinda bonde la mto Mara kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kutoka mugumu serengeti mkoani mara,mwanahabari wetu george marato,anayotaarifa zaidi.....Kauli hiyo imetangazwa mjini mugumu wilayani serengeti,na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh mizengo Peter Pinda,katika kilele za maadhimisho ya siku ya mara ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza nchini kwa kuhusisha nchi za Tanzania na kenya lengo likiwa ni kuweka mikakati ya pamoja ya kuhifadhi bonde la mto mara kwa sababu hiyo waziri mkuu mh mizengo pinda,amesema lazima serikali za nchi hizi mbili wakiwemo wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa bonde la mto mara kutokana na manufaa yake makubwa kwa wanyama aina ya nyumbu na hivyo kuwa kivutio kikubwa katika sekta ya utalii kwa hifadhi za Masai Mara nchini Kenya na hifadhi ya Taifa ya Serengeti hapa nchini ambayo ni moja ya maajabu saba ya Dunia. Akitoa salama za kutoka nchini Kenya, katibu mkuu wa wizara ya mazingira na maji ya nchi hiyo bw James Teko, wakiwemo wadau wanasaidia uhifadhi wa bonde la mto Mara, wamesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kwa kila mdau katika kulinda na kuhidhi bonde la mto Mara. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Mara ni mali yetu na urithi wetu tuitunze
No comments:
Post a Comment