Pages

Sunday, 22 September 2013

SAM WA UKWELI::"NILIUA BILA KUKUSUDIA" INANIUMIZA SANA


Sam ameeleza kuwa hakuna kitu kinachomuuma sana kama siku alipomdondosha mdogo wake chini na kumsababishia kifo kutokana na kuanguka kwake,msanii huyo amesema kuwa kisa hicho kilitokea wakati mama yake akiwa shambani na kumuacha sam na mdogo wake na ilipofika mchana sam aliyekuwa kambeba mdogo wake huku akitokea ndani akiwa kabeba uji wa huyo mtoto,ila kwa bahati mbaya sam alijikwaa na kudondoka chini na kumfanya yule mtoto alie sana hadi baba huyo wa kufikia wa sam alipokuja na kuanza kumfokea sam hadi mama yake alipokuja na kumnyonyesha mtoto na kulala ula usiku mtoto alianza kulia kwa staili ya kustuka ikapidi wampeleke hosptali ya mision na alipoangaliwa alionekana hana kitu ikabidi waondoke nae hadi kwa wataalamu wa jadi ila muda mfupi yule mtoto akafariki.

Sam anasema kuwa baada ya hapo baba huyo wa kufikia alisema sam kamuua mwanae maksudi na kuleta mtafaruku mzito katika familia yao jambo lililosababisha ndoa hiyo kuvunjika  na wakarudi kwa bibi yake mzaa mama  na ndipo walipokuja kushangaa baada ya  baba yao mzazi ambae waliambiwa kafa kurudi nyumbani akiwa mzima kabisa na ndio safari ya kuja dar kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment