KIKOSI CHA DEFENDER CHA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI KIKOSI CHA POLISI MAGOMENI |
WAZEE WA KAZI MARA BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI YA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI NA KUFANIKIWA KUMUUA MMOJA |
MOJA KATI YA WATU WANAODAIWA KUPORA FEDHA VINGUNGUTI BAADA YA KUUAWA NA POLISI |
Tukio hilo limetokea leo saa tano asubuhi maeneo ya SUKITA na taarifa kutoka eneo la tukio zinasema,watu hao wanadaiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa katika duka moja la jumla na reja reja eneo la vingunguti jijini Dar es Salaam.
Taarifa zinasema majambazi hayo yalikuwa manne na yalikuwa na usafiri wa pikipiki na mara baada ya kupora wananchi walianza kuyazingira ndipo mmoja wapo aliyeshika mfuko wa fedha walizopora akaanza kuzirusha kwa wananchi na walivyoanza kuzigombea pesa hizo ndipo yakapata mwanya wa kutoroka eneo la tukio.
Hata hivyo taarifa ziliwafikia polisi ambao walikuwa doria na walipewa taarifa kuwa yanaelekea njia ya sukita na walipowawekea mtego wakanasa,na ndipo katika harakati za kuwakamata walianza kuwarushia risasi polisi,ndipo moja kati yao, alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo na mengine matatu yakatokomea kusikojulikana
CREDIT. Abdalla mwaipaya blogspot.
No comments:
Post a Comment