Pages

Wednesday, 18 September 2013

MWINJILISTI MWANAMKE KIZIMBANI KWA KUWATUNZA WAHAMIAJI HARAMU

         



Baadhi ya raia wa Nigeria wanaodaiwa kutunzwa na  Mwinjilisti mwanamke  mwenye kibali cha kazi hiyo, Blessing  Dangana katika huduma ya Life Changer  Chapel iliyoko Sinza  jijini Dares Salaam, wakitoka  nje ya Mahakama ya  Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo huku wengine wa kijificha sura zao.Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo

Mwinjilisti  mwanamke  kutoka nchini Nigeria ambaye ana kibali cha kazi ya uinjilisti  katika huduma ya Life Changer  Chapel  iliyoko Sinza  jijini Dares Salaam, Blessing  Dangana, anayedaiwa kuwatunza raia wa Nigeria watano ambao wanatoa huduma hiyo bila kibali maalum akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo jana.



 



Baadhi ya vijana wanaodai kuwa wanatoka mkoa wa Kigoma  wakiwa wajaza fomu  jana ambao taarifa zao zinaendelea kuchunguzwa  kama  kweli ni Watanzania wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dares Salaam.


Gari la Idara ya Uhamiaji likiwa limebeba baadhi ya watuhumiwa hao mara baada ya kutoka mahakamani.

 NA MAGRETH KINABO 
– MAELEZO

OFISI  ya Uhamiaji mkoa wa Dares Salaam imemfikisha mahakamani Mtanzania anayedaiwa kuwatunza raia watano kutoka   Nigeria  wanaoishi nchini bila kibali halali baada ya kuwapiga na kuwazuia kufanya kazi maofisa wa uhamiaji kwenye ofisi za Serikali.

 Hayo yalisemwa leo na  Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Dares Salaam, Grace  Hokororo wakati akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari –MAELEZO   ofisini kwake ambapo alisema Mtanzania huyo alifikishwa leo(jana) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu baada ya kutenda kosa hilo jana majira ya saa 1:00 jioni.

 Alimtaja Mtanzania huyo kuwa ni Christopher Kanyala mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati miaka 29 hadi 34 mkazi wa Sinza na anadaiwa kuwa aliwaHI kutumikia Jeshi la Polisi nchini, ambapo kesi yake na raia hao watano wa Nigeria itatajwa kesho katika mahakama hiyo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo , Grace aliwataka wananchi   wasipende kuishi na raia ambao ni wageni na hawajaripoti katika ofisi za uhamiaji kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria. Huku akiwataka raia wa kigeni kuripoti katika ofisi hizo mara baada ya kuwasili nchini  ili waweze kufuata  taratibu za kisheria.
Aidha  alisema  operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu inaendelea vizuri.  Grace alisema kwa upande wa wahamiaji haramu kutoka Malawi walijitokeza kwa hiari mpaka leo mchana idadi yao imefikia 1,863 tangu zoezi hilo lilipoanza.
Aliongeza kuwa opresheni hiyo imehusisha mataifa 31 ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Italia, Singapore Ethiopia,Libya Yemeni,Somalia,Komoro, Ujerumani, Afrika Kusini,Uturuki, Nigeria, Cameroon,Liberia na Bokinafaso., Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo(DRC) na India.

 Alisema jumla ya raia hao wa mataifa mengine waliokamatwa ni 502.

CHANZO: MICHUZI

No comments:

Post a Comment