Hirizi iliyokuwa imeandaliwa na ndugu wa mtuhumiwa mmoja wa kesi ya
mauaji ambayo alifanikiwa kuishika mkononi kwa lengo la kwenda kumrushia
hakimu Mahakama ya hakimu mkazi Tabora ikiwa ni hatua ya kujinasua
katika kesi hiyo ambayo Upelelezi wake umechukua muda mrefu kiasi cha
kumfanya mtuhumiwa kutumia hatua nyingine mbadala.Hata hivyo mtuhumiwa
huyo ambaye jina tunalihifadhi wakati akiingia chumba cha hakimu kwa
ajili ya kesi inayomkabili alishindwa kutekeleza adhma yake kama
alivyoelekezwa na hivyo kuamua kuitupa chini kabla.
Licha ya kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria kuanza kusikiliza
shauri hilo lakini mtuhumiwa pamoja na ndugu zake waliamini kuwa
chochote kinaweza kufanyika baada ya kuirusha Hirizi hiyo kwenye Meza ya
Hakimu