Askari Polisi watatu wa Operesheni Kimbunga wamefariki dunia jioni ya juzi mjini Kahama baada ya kupata ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Muleba mkoani Kagera kuelekea makambako mkoani Njombe.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Sungamile Kata ya Kagongwa wilayani Kahama wakati dereva wa gari hilo PF3270 PC Yusuph, akijaribu kumkwepa Bibi Kizee mmoja huku gari likiwa kwenye mwendo kasi na hivyo kumshinda na kupinduka.
Majeruhi wanane wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama wakiwemo askari polisi sita na Maafisa Uhamiaji wawili, huku magari yanayosafirisha askari kurudi vituoni kwao yakizuiliwa kuendelea na safari na kulala Kahama.
No comments:
Post a Comment