Mwili wa marehemu Asha Rashid Hussein ulivyokutwa chumbani baada ya kifo chake.
Asha Rashid Hussein mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es salaam amekutwa amekufa kwenye chumba cha biashara ya chakula.
Siku ya tukio walidai kuwa akiwa ameanza kukanda unga wa chapati, alijifungia ndani ya chumba hicho kilichokuwa na jiko la mkaa ambapo alianza kupika bila watu kufahamu kuwa ndani kulikuwa na mtu.
Siku ya tukio walidai kuwa akiwa ameanza kukanda unga wa chapati, alijifungia ndani ya chumba hicho kilichokuwa na jiko la mkaa ambapo alianza kupika bila watu kufahamu kuwa ndani kulikuwa na mtu.
Ilipofika muda wa saa nne bila kufunguliwa alifika kijana mmoja
ambaye huwa anafanya naye kazi na kushangaa kuona hapajafunguliwa
alipojaribu kufungua, aligundua kuwa mlango umefungwa kwa ndani, akaenda
kumuita mama mwenye nyumba ili wafungue mlango walipofungua waligundua
kuwa Asha alikuwa tayari ameshafariki na ndio wakatoa taarifa polisi
Mwanananyamala ambao walifika eneo la tukio na kuamuru mwili uchukuliwe
na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi.
Jamaa na majirani waliofika kushuhudia tukio hilo.
Diwani wa Mwananyamala kwa Manjunju eneo lilipotokea tukio hilo, Ally
Haroub alisema kuwa marehemu alikuwa akimfanyia kazi mwajiri wake,
Mwidini Isaac (picha kubwa) ambaye siku hiyo alikuwa nje ya mji lakini
alipofahamishwa aliwatafuta ndugu na kuwafahamisha kilichomtokea ndugu
yao.
Diwani huyo alieleza kuwa kwa mujibu wa daktari wa Mwananyamala
marehemu alifariki kutokana na kukosa hewa baada ya kuvuta gesi ya mkaa
aliokuwa akipikia alipojifungia kwani ‘flame’ hiyo haikuwa na hewa
kutokana na kukosa dirisha.
No comments:
Post a Comment