Friday, 23 August 2013

WAZIRI NCHIMBI AWAVUA MADARAKA MAOFISA WA JESHI LA POLISI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya Uchunguzi wa Matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari Polisi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya Uchunguzi wa Matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari Polisi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na tukio la gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kutumika katika uhalifu (ubebaji bangi) katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Polisi Mkoa wa Morogoro kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kumbambikizia mfanyabiashara kwa lengo la kupata fedha na Mauaji ya mfanyabiashara wa Wilaya ya Kasulu yaliyofanywa na Askari wawili wa Jeshi la Polisi. Taarifa hiyo ameitoa katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo.
 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na mali zao.


Alisema amewachukulia hatua Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na Mei, 2013.


Waziri Nchimbi aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta Jamal Ramadhan, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Dumila Inspekta Juma Mpamba na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho na kumsimamisha kazi Inspekta Isaack Manoni.


Alifafanua kuwa Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro alivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maafisa walio chini yake ambao walikamatwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 540 kwa kutumia gari la polisi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!