Tuesday, 27 August 2013

WALIOPITISHA ‘UNGA’ WATIMULIWA

              
                                                                    
Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) picha ya dawa za kulevya zilizokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hivi karibuni.
*WAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA UWANJA WA NDEGE

HATIMAYE maofisa usalama wanne katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wamepewa barua zao za kuachishwa kazi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyemba kuagiza waachishwe kazi mara moja kutokana na kutuhumiwa kuhusika kwao katika kusaidia watu kusafirisha dawa za kulevya kilo 180.
Maofisa hao kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe ni Yusufu Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwana, baada ya kukabidhiwa barua zao wamepigwa marufuku wasikanyage katika uwanja huo.
CHANZO GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!